KAMPALA,UGANDA
WAKIMBIZI zaidi ya elfu tatu wanaokimbia mapigano ya kikabila nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wameripotiwa kuvuka mpaka na kuingia nchini Uganda baada ya mpaka wa nchi hiyo kufunguliwa kwa muda wa siku tatu.
Msemaji wa Shirika la kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR nchini Uganda Duniya Aslam Khan aliwaambia waandishi wa habari wa Xinhua kuwa wakimbizi 3,056 wanaotafuta hifadhi ambao walikuwa wamekwama kwenye eneo la mpakani kati ya Uganda na mashariki mwa DRC tangu mwezi Mei, wamevuka mpaka na kuingia kwenye eneo la Zombo, kaskazini magharibi mwa Uganda.