NA SIMAI HAJI,MCC
WANACHAMA wa chama cha Mapinduzi CCM wametakiwa kushikamana na kuwa pamoja, ili kujenga nguvu imara ya kukipa ushindi chama hicho siku hadi siku.
Katibu wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa KusiniSuleiman Mzee Charas, aliyasema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Paje uliofanyika Kitogani wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Alisema suala la umoja na mshikamano kwa wanachama cha Mapinduzi ndio silaha pekee ya kukipa ushindi wa kishindo chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.
Aidha alisema kuwa CCM ni moja na wanachama wake ni wamoja hivyo ni vyema kuondokana na utabaka katika chama kwani kufanya hivyo kutaongeza hamasa na upendo kwa wanachama wake.
Nae Katibu wa CCM Wilaya ya Kusini, Hafidh Mkadam alipongeza uongozi wa jimbo kwa kumaliza salama upigaji wa kura ya maoni ya kutafuta wagombea wa ubunge na Wawakilishi kupitia chama hicho huku wakidumisha amani na utulivu wakati zoezi hilo lilivokua lkiendelea muda wote.