RAMALLAH, PALESTINA

WANAJESHI wa Israeli walimpiga risasi na kumuua kijana wa kipalestina katika ukingo wa Magharibi, imesema wizara ya afya ya Palestina.

Kijana huyo alipigwa risasi na askari wa Israeli katika kijiji cha Kifl Haris karibu na mji wa Salfit katika Ukingo wa Magharibi, ambapo alifariki baadaye kutokana na jeraha kubwa shingoni mwake, wizara hiyo ilisema.

Tukio hilo lilitokea baada ya kutokea mapigano kijijini hapo kati ya askari wa Israeli na vijana wa Palestina, vyanzo katika kijiji hicho vilisema.

“Wanajeshi wa Israeli walitumia silaha za moto kwa vijana wa Palestina ambao walitupa mawe kwa jeshi la Israeli ambalo lilishambulia kijiji hicho siku ya Alhamisi”, vyanzo viliongezea.

Hata hivyo, jeshi la Israel hadi sasa halijasema chochote kuhusiana na tukio hilo.

Nae Waziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Ishtaye aliishutumu Israeli kwa kitendo cha kumuua kijana huyo wa Palestina.

“Mwanajeshi huyo wa Israeli anawajibika kikamilifu kwa mauaji ya kijana wa Palestina huko Salfit bila sababu yoyote,” alisema Ishtaye.

Aliongeza kwamba “mauaji hayo ni sehemu ya uhalifu ambao wanajeshi wa Israeli wanafanya dhidi ya Wapalestina.