NA AHMED MAHMOUD, ARUSHA

WANANCHI zaidi ya elfu tatu kutoka Kijiji Cha Kikuletwa kata ya Mbuguni wilayani  Simanjiro mkoani Manyara wanatarajiwa kunufaika na  mradi wa kisima cha maji unaoanzia mkoani Manyara kwenda Arusha.

Wakizungumzia kuhusiana na mradi huo wananchi hao Janeth Apaeli na Ida Nanyaro ,walisema kuwa mradi huo umekuja muda muafaka ambao wananchi hao walikuwa wakikumbana na changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji.

Walisema kuwa, kukosekana kwa maji katika eneo hilo limekuwa ni changamoto ya Muda mrefu, kwani wanawake ndio wamekuwa wakipata shida kutokana na kuamka usiku kufuata maji, jambo ambalo linahatarisha maisha yao kutokana na usalama kuwa mdogo.

“Kwa kweli tunashukuru Sana serikali kwa kuleta mradi huu katika eneo hili, mradi ambao umekuwa ni kilio cha muda mrefu kutokana na adha tunayoipata” alisema .