NA FATMA AYOUB, MCC

WANANCHI wa Wilaya ya Magharibi ‘A’ wametakiwa kucha tabia ya kutupa taka ovyo ikizingatiwa kipindi hiki, ili kuepusha maradhi mbali mbali ikiwemo Kipindipindu.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Jamii, Afya na Mazingira wa Manispaa ya Wilaya hiyo, Asha Bakari, alipokuwa akizumgumza na gazeti hili huko ofisini kwake Malindi Mjini Unguja.

Alisema kumekuwa na baadhi ya wananchi ambao hutupa taka maeneo yasio husika ikiwemo chini ya nyumba za makaazi ya watu, hali inayopelekea uchafuzi wa mazingira na kuhatarisha afya za watu.

Alifahamisha kuwa wananchi wawe makini juu ya suala la uchafuzi wa mazingira kwani lina madhara makubwa kwa jamii, ikiwemo maradhi hatari ya mripuko.

“Lazima tuwe makini katika kipindi cha mvua kwani ndipo yanapo jitokeza marandhi ya mengi tusipoweka mazingira safi katika Wilaya yetu tunayakaribisha maradhi” alisema.