NA HUSNA SHEHE

JESHI la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, limewakamata wanawake 28 kwa tuhuma ya kujihusisha na biashara ya kuuza miili yao (ukahaba) katika Manispaa ya Mji wa Zanzibar.

Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Awadhi Juma Haji, akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya matukio ya wiki yaliyotokea katika mkoa wake, alisema wanawake hao walikamatwa Julai 13, mwaka huu, majira ya saa 6:30.

Alisema  baada ya kufanya msako katika maeneo tofauti ya Mji wa Zanzibar, wanawake hao walikamatwa wakifanya biashara ya ukahaba kwa kujiuza katika eneo la Maisara.

Kamanda Awadhi, amewataka wanawake wanaofanya biashara ya ukahaba waache biashara hiyo na wajishughulishe na kazi zenye tija kwao kwani biashara hiyo haina faida bali kuzidisha maambukizi ya maradhi hatari.

Siku hiyo majira ya saa 7:00 usiku alisema  jeshi hilo limewakamata watu wanne kwa kosa la kukiuka masharti ya leseni ya biashara ya Baa kwa kuuza bila ya kwa na leseni ambayo inawataka ifikapo saa 6:00 usiku wafunge baa zao

Hivyo amewataka wafanya biashara ya baa wafuate masharti wanayopangiwa.