NA TATU MAKAME

MKUU wa Utawala wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Zanzibar, Asya Sharif Omar, amewataka vijana wa kike kuacha kubezana wakati kundi hilo linapo kwenda majimboni kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kwenye nafasi za uongozi.

Aidha amewataka vijana wa kike kujitokeza majimboni kugombania nafasi za uongozi wakati ukifika, ili kufikia usawa wa 50 kwa 50 kwenye nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Sharif alisema hayo wakati alipozungumza na Zanzibar Leo Ofisini kwake Gymkhana Wilaya ya Mjini, ambapo alisema wapo wanaobeza wanawake wanapofika majimboni kuomba ridhaa ya kuchaguliwa nafasi za uongozi huwawaunga mkono wanaume pekee, jambo linalosababishia kukosa majimbo.

“Umefika wakati wanawake wanaona bora wakawasaidie wanaume lakini sio wanawake tuache tabia hii kwani inavunja moyo”,alisema.