MOSCOW,URUSI

MAELEFU  ya raia wa Urusi wameandamana katika mji wa mashariki ya mbali ya taifa hilo wa Khabarovsk wakipinga kukamatwa ghafla kwa gavana wa eneo hilo ikiwa ni wiki ya tatu mfululizo.

Gavana huyo Sergei Furgal alikuwa kuzuizini mjini Moscow tangu alipokamatwa Julai 9 kwa madai ya mauaji.

Gavana huyo maarufu anatuhumiwa kujihusisha na visa kadhaa vya mauaji ya wafanyabiashara mnamo mwaka 2004 na 2005 wakati yeye mwenyewe alipokuwa mfanyabiashara aliyejihusisha na biashara ya mbao na chuma.

Hata hivyo aliyakana madai hayo,waandamanaji hao wanahisi kwamba madai dhidi ya gavana huyo hayana ukweli wowote na wanataka kesi hiyo kuendeshwa kwa uwazi katika mji huo wa Urusi ulio karibu na mpaka na China.