BERLIN,UJERUMANI

MAWAZIRI wa Afya Ujerumani wameamua kuwa wasafiri wanaoingia nchini humu kutoka nchi zilizo na maambukizi mengi kufanyiwa vipimo vya virusi vya corona katika viwanja vya ndege.

Kwa mujibu wa  shirika la habari la Ujerumani DPA, mawaziri hao pamoja na waziri wa afya wa Shirikisho Jen Spahn walikubaliana kuhusiana na vipimo hivyo vya lazima wakati wa kikao cha video walichokifanya ila uamuzi wa mwisho bado haujatiwa saini.

Mazungumzo zaidi kuhusiana na suala hilo yalipangiwa kufanyika jana.

Hadi sasa wasafiri wanaoingia Ujerumani kutoka nchi zenye hatari kubwa ya kupata maambukizi wanalazimika kujiweka karantini kwa siku kumi na nne ingawa hatua hiyo ilikuwa ngumu kuitekeleza.

Kulingana na shirika la kudhibiti magonjwa Ujerumani nchi zote za Ulaya sasa hivi ni nchi ambazo zina hatari kubwa.

Watu wanaoingia Ujerumani kutoka nchi zilizo na idadi ndogo ya maambukizi watalazimika kujitenga kwa siku kumi na nne.