KAMPALA,UGANDA

LICHA ya kuwepo kwa matumaini ya kupatikana kwa dawa ya kutibu maradhi ya Covid-19 lakini imesisitizwa kuwa kunahitajika uchunguzi Zaidi kufanyika juu ya ubora wa dawa hiyo kabla ya kuanza kutumika kwa umma.

Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Magonjwa ya kuambukiza,Dk Andrew Kambugu,alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuibuka taasisi nyingi zinazotengeneza dawa ya amaradhi hayo.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema ilikuwa ina chanjo ya salama ya virusi vya corona kufuatia majaribio ya kliniki kwa kikundi cha kujitolea.

Kulingana na shirika la habari la AFP, wizara hiyo ilisema watu 18 walishiriki katika utafiti wa dawa hiyo walifanikiwa bila ya kupata athari yoyote ya kiafya.

Kesi zaidi ya milioni 13.5 za virusi vya corona zilithibitishwa na vifo 587,779 viliripotiwa ulimwenguni kote.

Dk Ekwaro Obuku, Rais wa zamani wa Chama cha Madaktari wa Uganda, alisema chanjo hiyo ni maendeleo mazuri katika mapigano ya Covid-19.