BAGHDAD, IRAQ
WATU wenye bunduki wasiojulikana waliwapiga risasi watu wa familia sita katika kijiji kimoja kilichoko mkoa wa Salahudin nchini Iraq.
Kwa mujibu wa chanzo cha polisi wa mkoa huo, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku wa Ijumaa wakati watu hao wenye silaha walipovamia nyumba ya Ali Mukhlif.
Mkuu wa utawala wa kijiji cha Samoum kaskazini magharibi mwa mji wa Samarra, kilomita 120 kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Iraq Baghdad, Mohammed al-Bazi aliliambia Xinhua.
“Washambuliaji walishambulia kwa silaha za moto na kumpiga risasi Mukhlif, huku wanawe wanne na mpwa wake wakiwahi kukimbilia katika bustani ya iliyokuwa karibu, al-Bazi alisema.
“Kikosi cha usalama cha Iraqi kilifika eneo la tukio na kuanza uchunguzi juu ya tukio hilo, aliongeza.
Shambulio hilo lilikuja wakati wanamgambo wa Islamic State (IS) wakiwa wameongeza mashambulio yao kwa vikosi vya usalama na raia katika majimbo ya zamani ya ISI yanayodhibitiwa na IS na kusababisha kuuawa na kujeruhi kwa watu kadhaa.
Hali ya usalama nchini Iraq imekuwa ikiboreka tangu vikosi vya usalama vya Iraqi vilipowashinda kikamilifu wanamgambo wa IS kote nchini humo mwishoni mwa mwaka 2017.