NA LAYLAT KHALFAN

BARAZA la Manispaa Mjini limesema, limewashikilia wafanyabiashara 11 wa wanaotoa huduma ya chipsi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar kwa kukiuka taratibu za afya kwa mlaji kwa kulisha watu viporo vya vyakula hivyo.

Mkurugenzi wa Baraza hilo, Said Juma Ahmada, alitoa takwimu hiyo mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua vioksi vya wanao uza bishara hiyo katika maeneo mbali mbali ya Manispaa ya mjini ambayo inalenga zaidi kuzingatia afya kwa mlaji wa bidhaa hiyo na kuwa katika hali ya ubora.

Alisema kwa kawaida wafanyabiashara wengi wa vioksi wenye kuuza chipsi katika maeneo mbali mbali ya mji  wanashindwa kufuata taratibu za afya, jambo linalosababisha kuwepo kwa maradhi ya mripuko.

 “Mfanyabiashara bila kuzingatia taratibu za afya  hususan biashara ya chukula hatuwezi kumuacha kwani wapo wanafikia hatua wanawauzia wateja chipsi za jana chakula ambacho hakina ubora hili hatutolivumilia lazima tuchukue hatua”, alisema.