ADDIS ABABA, ETHIOPIA
WATU wawili wamepigwa risasi na kufariki na wengine saba wamejeruhiwa wakati wanajeshi walipofyatua risasi dhidi ya waombolezaji waliotaka kuhudhuria mazishi ya muimbaji maarufu nchini Ethiopia.
Muimbaji huyo ambae kuuwawa kwake kulizusha ghasia ambazo zilisababisha kiasi watu 100 kuuwawa.
Hachalu Hundessa, kutoka katika kabila la Oromo, kabila kubwa nchini Ethiopia, alipigwa risasi na washambuliaji wasiojulikana katika mji mkuu Addis Ababa usiku wa Jumatatu, na kuzusha hali ya wasi wasi ikitishia kipindi cha mpito nchini humo cha demokrasia.
Muziki wake ulitoa sauti kwa hali ya ukandamizwaji na kutengwa kwa Waoromo kiuchumi na kisiasa katika miaka ya maandamano ya kupinga serikali ambayo ilimuingiza madarakani waziri mkuu Abiy Ahmed mwaka 2018.
Mazishi hayo yaliyotangazwa mubashara katika mtandao wa matangazo wa Oromia,yalifanyika katika mji anakotoka Hachalu wa Ambo, magharibi mwa mji mkuu Addis Ababa.