NA ARAFA MOHAMED

WINGI wa Wanafunzi katika Skuli ya Mkokotoni kusoma darasa   moja kunawahuzunisha Wazee, Walimu pamoja na Kamati ya Skuli hiyo na kuamua kukaa pamoja kulitatua tatizo hilo.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wakaazi wa shehia ya Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Mkoa wa Kaskazini Unguja, walisema wamekuwa wakiona wanafunzi wengi wanasoma darasa moja, jambo ambalo litapelekea wanafunzi hao kufanya vibaya katika masomo yao.

Walifahamisha kuwa, wamefanikiwa kuanza ujenzi wa banda lenye madarasa nane, ambalo litapunguza msongamano kwa wanafunzi hao kusoma darasa moja.

Aidha walisema, ujenzi huo wa madarasa manane ambao ulianza kujengwa na wao wenyewe,  lakini bado haujakamilika, hivyo wanaiomba Serikali kupitia Wizara husika kuwamalizia ujenzi huo ili kuhakikisha wanafunzi hao wanapata elimu katika mazingira mazuri.

“Upungufu wa madarasa ya kusomea kwa wanafunzi hao unapelekea wanafunzi, kutokufanya vizuri katika masomo yao na kusababisha usumbufu kwa mwalimu anapoingia darasani wakati wa kufundisha’. walisema.