TUNIS,TUNISIA
WAZIRI Mkuu wa Tunisia Elyes Fakhfakh amejiuzulu miezi mitano tangu alipochukua madaraka.
Hatua ya Fakhfakh inatishia kusababisha mkwamo wa kisiasa wakati taifa hilo la kaskazini mwa Afrika linajidhatiti kudhibiti uchumi wake usiporomoke kutokana na athari za janga la corona.
Fakhfakh alijiuzulu wakati mzozo wa kisiasa ukishamiri kati yake na chama cha siasa kali za Kiislamu Ennahdha ambacho ndicho kikubwa zaidi bungeni kuhusu madai ya mkwaruzano wa kimasilahi.
Ofisi ya Waziri Mkuu ilisema kwenye taarifa kuwa ili kuepusha mvutano kati ya asasi nchini humo waziri mkuu Elyes Fakhfakh aliwasilisha waraka wake wa kujiuzulu kwa Rais Kais Saied.