KIGALI,RWANDA

WAZIRI  wa Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnston Busingye, amesema kwamba hakuna mtu atakayeokolewa wala kulindwa katika harakati za kutaka uwajibikaji.

Alitoa kauli hiyo, wakati akizungumza na waandishi wa habari  katika makao makuu ya Wizara hiyo huko Kigali.

“Tunapaswa kuzoea ukweli kwamba viongozi huitwa na wachunguzi na kuhojiwa au hata kufungwa gerezani … hii ni kwa sababu ya serikali inayohusika na uwajibikaji,” Busingye alisema.

Alisema kuwa uwajibikaji ni dhamana ya msingi ambayo chama hicho kinajengwa na lazima ukumbatiwe na viongozi wote.

Busingye alisema  serikali inaweka kipaumbele zaidi katika kupigana na uhalifu wa kifedha kwa sababu ya athari waliyo nayo kwenye uchumi na ustawi wa watu wa Rwanda.

Alitaja ufisadi huo kuwa ni , matumizi ya fedha za umma, ukwepaji kodi, utapeli wa pesa, miongoni mwa makosa mengine ya kifedha, kama uhalifu ambao unachelewesha maendeleo ya nchi ikiwa hayatasimamiwa.

Wakati huo huo, watu wasiopungua tisa wapo mahabusu kuhusiana na utapeli wa pesa kiasi cha Rwf9 bilioni ambayo ilikusudiwa kununulia mbolea kwa wakulima kote nchini.

Ilibainika  kwamba idadi ya mbolea ambayo walidai wamesambaza ilikuwa chini sana kuliko ile ambayo walipewa wakulima.

Kesi hiyo ina watu 12,tisa walifungwa, wakati watatu waliachiliwa lakini bado wana deni la jinai na uwezekano mkubwa wa kushitakiwa kulingana na Bahorera.