NA NASRA MANZI

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali kupitia Idara ya Michezo na  Utamaduni, imeombwa kuchagua timu ya michezo ya ndani ya riadha, kwa ajili ya kupata timu nzuri katika mashindano ya Umisseta itakayoweza kuleta ushindani.

Kauli hiyo imetolewa na kocha wa michezo mitupo ikiwemo kurusha kisahani, Tufe na Mkuki Ali Seif Juma ‘ Jangal’ alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Alisema ni vyema wanafunzi watakapomaliza mashindano ya Elimu Bila Malipo  kuchaguliwa timu hiyo kwani wakati huo tayari vipaji vingi vimeonekana,kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Umisseta.

Pia alisema jambo hilo litasaidia kupata wachezaji wenye viwango vya timu na kupata timu bora ambayo italeta ushindani kama timu nyengine.