NAIROBI,KENYA
WIZARAN ya Afya nchini Kenya imesema kuwa taifa linaelekea katika kipindi cha maambukizi ya juu zaidi kati ya Mwezi Agosti na Septemba huku watu wengine kumi na mmoja wakithibitishwa kufariki dunia na kufikisha idadi jumla ya waliofariki kutokana na Covid-19 kuwa watu 274.
Katibu wa Utawala wa Wizara ya Afya Dakta Mercy Mwangangi alithibitisha kuambukiwa virusi vya korona watu 667 kutokana na vipimo vya sambuli 5,075 vilivyopimwa kwa kipindi cha saa ishirini na nne,idadi ambayo ilifikisha jumla ya maambukizi nchini kuwa 16,268 na sambuli 266,102.
Miongoni mwa walioambukizwa 657 ni Wakenya huku kumi wakiwa raia wa mataifa ya kigeni. Mtoto mchanga mwenye umri wa mwezi mmoja na mzee wa miaka 92 ni miongoni mwao.
Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa visa vya maambukizi ambapo visa 387 viliripotiwa, Kiambu 40, Mombasa visa 26, Machakos 47, Kiajiado 79, Nakuru, 15, Uasingishu 14, Garissa 11, Busia tisa , Kilifi na Turkana visa sita , Makueni, vitano, Wajiri vitano huku Bomet, Narok, Bungoma na Nyamira vikiwa na visa kimoja kimoja.
Watu wengine 311 walipona huku idadi jumla ya waliopona Covid-19 ikifikia watu 7,446. Miongoni mwao 166 walikuwa wakitibiwa nyumbani huku 145 ni wale waliokuwa wakitibiwa hospitalini.
Wizara ya Afya kwa mara nyengine iliwashauri Wakenya kuzingatia maagizo ya kukabili maambukizi hasa taifa linapoelekea katika msimu wa maambukizi ya juu katika ya Mwezi Agosti na Septemba.