KINSHASA,DRC

OFISI  ya Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika imeeleza wasiwasi wake kutokana na mripuko wa 11 wa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mwezi Juni mwaka huu, DRC ilitangaza kumalizika kwa mripuko wa Ebola kwenye sehemu ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, lakini mlipuko mpya wa ugonjwa huo ulitokea mwezi huo huo kwenye mkoa wa Ikweta, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Taarifa hiyo inasema, kuanzia tarehe Mosi mwezi Juni, maambukizi yalisambaa kwenye maeneo sita ya mkoa wa Ikweta.

Hadi sasa  mwezi Julai, mkoa huo uliripoti kesi 56, wakiwemo watu 53 waliothibitika kuwa na virusi vya Ebola na wengine watatu wanaohisiwa kuwa na maambukizi.