LONDON,UINGEREZA
SHIRIKA la afya duniani WHO, limesema kwamba kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona katika nchi kadhaa kumesababishwa na vijana wasiojali kujikinga.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus aliwatadharisha vijana kwamba wao pia wanawezwa kuambukizwa.
Tedros alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya video kwamba,ingawa idadi kubwa ya watu waliokumbwa na maambukizi ni watu wazima ambao tayari wana maradhi sugu, vijana pia wamo katika hatari ya kuambukizwa virusi vya corona.
Mpaka sasa watu milioni 17 wamekumbwa na maambukizi hayo duniani kote na 670,000 wameshakufa.
Tedros alisisitiza kuwa vijana pia wanaweza kufa kutokana na maradhi ya Covid 19 na pia wanaweza kuwaambukiza watu wengine.
Mkurugenzi mkuu huyo wa shirika la WHO alisema kwamba maambukizi yaliongezeka katika nchi kadhaa kutokana na vijana kuregeza hatua za kujikinga na hasa sasa wakati wa kiangazi katika nchi za kaskazini ya dunia.