LONDON,UINGEREZA

MKURUGENZI wa Utekelezaji wa Programu za Dharura wa Shirika la Afya Duniani (WHO), amesema uzalishaji wa chanjo ya corona utachukua muda.

Dakta Mike Ryan alisema watafiti wako katika mchakato uliopiga hatua wa kuzalisha chanjo ya corona na utumiaji wa chanjo hiyo utachukua muda hadi mwanzoni mwa mwaka ujao.  

Alisema  utengenezaji wa chanjo kadhaa za corona umefikia  mara ya tatu ya majaribio na kwamba hakuna mara iliyofeli kati ya hizo na kuongeza kuwa, Shirika la Afya Duniani linafanya kila linalowezekana ili upatikanaji wa chanjo zenye faida dhidi ya virusi vya corona na kuzidisha uzalishaji wake.

Hadi sasa watu milioni 15 na 374,394 wameambukizwa virusi vya corona duniani na 630,211 wamefariki dunia kwa maradhi hayo ya Covid-19.

Aidha wagonjwa Zaidi ya milioni  tisa waliokuwa wamepatwa na maambukizi ya corona wamepona hadi sasa.