NEW DELHI,INDIA

SHIRIKA  la Afya Duniani WHO limeripoti kwa siku ya pili mfululizo juu ya kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona duniani, huku jumla ya visa vya vipya ikipindukia 259,000.

Kwa mujibu wa taarifa ya kila siku ya WHO maambukizi makubwa yalirikodiwa nchini Marekani, Brazil, India na Afrika ya Kusini.

Takwimu zilionesha kulikuwa na visa vipya 237,000 huku idadi ya watu wanaokufa kwa siku kutokana na ugonjwa wa COVID-19 ilipanda katika siku za karibuni ikilinganishwa  wiki chache zilizopita.

Kulingana na tarakimu zilizojumuishwa na shirika la habari la Reuters, visa vya virusi vya corona duniani vilipindukia milioni 14 na janga hilo tayari limewauwa karibu watu 600,000 katika kipindi cha miezi saba iliyopita.