NA MWANAJUMA MMANGA

WILAYA ya Magharibi ‘B’, Kati, Mjini na Kaskazini Pemba zimetajwa kuongoza kwa maambukizi ya kasi ya ugonjwa wa malaria kwa kipindi cha mienzi mitatu hivi sasa.

Maeneo hayo, yameonyesha kukuwa zaidi katika  shehia 20 ambazo zimeweza kutoa wagonjwa 1063,  ambapo kwa upande wa Magharib ‘B’ shehia ya Tomondo ina wagonjwa 100 inaongoza kwa wagonjwa wengi kwa wilaya zote

Akizungumza na Zanzibar Leo Ofisa Muhamasishaji kutoka Kitengo cha kumaliza Malaria Zanzibar, Ghanima Mbaraka Ussi, alisema shehia nyengine ni ya Mombasa yenye wagonjwa 36, Kiembe samaki wagonjwa 56 na Mbweni 68.

Alisema kwa upande wa  Wilaya ya Kati Jumbi wagonjwa 59 na Mjini Kiponda 75, Mkadara 72, Mpendae 64, Miembeni 58, Rahaleo 51, Kwahani 48, Gulioni 47, Kikwajuni juu 44, Kikwajuni Bondeni 43, Malindi 42, Mkunazini 41 Mkele 40, Mlandege 36 na Shangani 34, na  kwa upande wa Pemba Tumbe Mashariki 37.