WASHINGTON, MAREKANI

MAREKANI imerikodi visa vipya 55,000 vya virusi vya corona ndani ya saa 24 na hivyo kuifanya idadi ya maambukizi nchini humo kufikia 3,046,351.

Chuo Kikuu cha Johns Hopkins kilisema  kuwa Marekani ilirikodi vifo vipya 833 na kuifanya idadi jumla ya vifo kuwa 132,195.

Rais wa Peru, Martin Vizcarra alisema uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utacheleweshwa hadi mwezi Aprili mwaka ujao kutokana na janga la virusi vya corona.

Peru ilirikodi visa 312, 911 vya virusi vya corona na vifo 11,133.

Rais wa Serbia, Aleksandar Vucic aliwataka waandamanaji kuacha kuandamana ili kuzuia kuenea zaidi kwa virusi vya corona.

Bara la Afrika lilirikodi zaidi ya visa 508,000 vya virusi vya corona, baada ya Afrika Kusini kuthibitisha zaidi ya maambukizi mapya 10,000.