NA ZAINAB ATUPAE

UONGOZI wa timu ya Jumuiya ya Zanvarsity Alumni umesema unatarajia kukutana kuzungumza mambo mbali mbali, ikiwemo uchaguzi mkuu wa kutafuta viongozi wataongoza Jumiya hiyo.

Akizungumza na gazeti hili katibu wa timu hiyo Ameir Mohamed,alisema  kikao hicho kinatarajiwa kufanyika Jumamosi mwezi huu.

Alisema mbali na kujadili mkutano mkuu ambao hufanyika kila baada ya miaka mitatu watazungumza mechi za kirafiki ambazo hucheza kila wiki.

Alisema uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Disemba mwaka huu,lakini taarifa zitatolewa baada ya kumaliza kikao chao wiki hii.

Alisema kwa upande wa mechi za kirafiki wanatarajia kucheza kwa kila jumapili.

Aidha akizungumzia mechi zao ambazo wanacheza kwa kila mwaka na kwenda vijijini kutoa elimu walisema wanatarajia kufanyika Disemba mwaka huu.

Alisema hadi muda huu bado hawajajua sehemu gani watakwenda kutoa elimu hiyo na kucheza mechi ya kirafiki,lakini matarajio yao ni kucheza Mkoa wa Kaskazini Unguja.

“Mwaka huu tutanata kuelekea Kaskazini maana miaka yote tuliofanya tunaelekea Kusini na wilaya ya Kati Unguja”alisema.