NA JAALA MAKAME HAJI, ZEC

TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) itaanza zoezi la kugawa vitambulisho vya kupigia kura kuanzia kesho kwa wilaya zote za Unguja baada ya kukamilika kwa ugawaji huo katika wilaya za Pemba wiki iliyopita.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa tume hiyo Thabit Idarous Faina akizungumza na watendaji walioteuliwa kusimamia kazi hiyo vituoni alisema ZEC imeandaa utaratibu maalum utakaorahisisha zoezi hilo kufanyika kwa urahisi zaidi.

Mkurugenzi Faina, aliwataka watendaji hao kutoa elimu ya kutumia huduma ya mtandao wa Zantel kwa wapiga kura ambayo itawawezesha wapiga kura wanaokwenda kuchukua vitambulisho vyao kupata huduma hiyo kwa haraka zaidi na bila ya usumbufu.

“Kwa kutumia mtandao wa Zantel unaweza kupiga *152*29# ili kujua kibox ambacho kipo kitambulisho chako cha kupigia kura,” alifafanua Faina.

Aidha Faina alisisitiza kuwa, malengo ya tume hiyo ni kuendesha uchaguzi mkuu utaozingatia misingi ya haki, uhuru na uwazi.

Naye Mkuu wa Kurugenzi ya Elimu ya Wapiga Kura, Habari na Mawasiliano kwa Umma Juma Sanifu Sheha aliwataka watendaji hao kuifanya kazi hiyo kwa uadilifu, uaminifu na umakini wa hali ya juu ili kusaidia kuondosha malalamiko baina yao.

Wakizungumza katika mafunzo hayo Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Mjini Safia Iddi Muhammad na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Magharibi “B” Fatma Gharib Haji, waliasa watendaji hao kutumia lugha nzuri wakati wanapokuwa vituoni kutoa huduma hiyo.

Aidha waliwakumbusha umuhimu wa kuzingatia sera ya jinsia na ushirikishwaji wa makundi ya kijamii ya mwaka 2014 iliyoanzishwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ambayo inawaelekeza kuwapatia fursa ya kwanza watu wenye mahitaji maalum. Watendaji walioteuliwa kusimamia ugawaji wa vitambulisho katika vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga kura kwa kazi ya uandikishaji iliyopita walipongeza utaratibu uliowekwa na tume katika kutoa