MOGADISHU,SOMALIA
RAIA kumi na Ofisa mmoja wa Polisi waliuawa katika shambulio la bunduki na bomu lililofanywa na wapiganaji wa kundi la Al shabaab katika hoteli iliyoko ufukweni mwa mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Msemaji wa Wizara ya habari Ismael Mukhtaar Omar,alisema maofisa wa usalama walitumia muda wa masaa manne kulidhibiti tena eneo la tukio,baada ya wapiganaji watano kuvamia hoteli ya Elite.
Kulingana na mashuhuda,shambulio hilo lilianza kwa mripuko mkubwa wa bomu na watu kukimbia kutoka eneo la tukio, wakati milio ya risasi ikisikika kutoka hoteli ambayo mara nyingi hutembelewa na maofisa wa Serikali.
Kundi la Al-Shabaab limedai kuhusika na shambulio hilo. Wiki iliyopita wapiganaji wanne wa kundi hilo waliuawa na vikosi vya usalama vya Somalia.