KABUL, AFGHANISTAN

SERIKALI ya Afghanistan imeanza kuwaachia huru wafungwa wa mwisho wa kundi la Taliban kutoka kundi la wafungwa 400 ambao wanamgambo hao wanataka waachiwe kabla ya kukubali kuanza majadiliano ya amani.

Serikali ilikubali kuwaachia huru wafungwa sugu 400 baada ya ushauri kutoka Baraza la wazee pamoja na viongozi wengine wa jamii, linalofahamika kama Loya Jirga.

Msemaji wa baraza la usalama la taifa, Javid Faisal alisema Serikali  iliwaachia huru wafungwa 80 wa Taliban kutoka idadi ya wafungwa 400 ambao Loya Jirga iliidhinisha kuwachia,ili kuharakisha mazungumzo ya moja kwa moja na kusitisha mapigano nchi nzima.

Hata hivyo, hakusema lini kundi jengine la wafungwa 320 litaachwa huru.