KINSHASA,DRC

GAVANA wa Kivu Kusini alisemaNdege iliyokuwa imebeba watu wanne imeanguka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ndege hiyo,iliyokuwa ya Kampuni ya Agefreco, ilikuwa njiani kuelekea Bukavu huko Kivu Kusini kutoka Kalima katika mkoa wa Maniema.

“Nimejifunza tu juu ya ajali ya ndege ya Kampuni ya Agefreco na watu wanne,uchunguzi utatoa chanzo cha ajali.Ninashiriki maumivu ya familia zinazoomboleza na ninatoa pole sana,”alisema gavana wa Kivu Kusini Théo Kasi Ngwabidje.

Ndege hiyo ilikuwa imeondoka kwenye uwanja wa ndege wa Kinkungwa na iliripotiwa kupotea baada ya dereva kuzungumza na mnara wa kudhibiti Kavumu huko Bukavu dakika saba kabla ya kutua.

Ndege hiyo ndogo ilikuwa imebeba abiria wawili,wafanyakazi  wawili na mizigo.

Msemaji wa Kivu Kusini Desiree Kyakwima alisema Ndege hiyo bado haijapatikana lakini la ajali linaloshukiwa ni msitu mkubwa.