NA MWANAJUMA MMANGA
JESHI la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja linamshikilia kijana mmoja mkaazi wa Kwarara kwa kupatikana na misokoto 16 ya majani makavu yanayoaminika kuwa ni bangi huko viwanja vya skukuu Bwejuu Mkoa huo.
Kamanda wa polisi wa Mkoa huo, Suleiman Hassana Suleiman, akithibitisha kukamatwa kijana huyo, Hasaan Shamate Hassan (22) mkaazi wa Kwarara Wilaya ya Magharib ‘B’ Unguja.
Alisema kijana huyo amekamtwa wakati jeshi hili likiendesha operesheni maalum katika maeneo tofauti ya kupambana na vitendo vya wahalifu, wauzaji, na wasambazaji wa dawa za kulevya katika kipindi hiki cha skukuu.
Aidha alisema wamefanya doria maeneo ya Bwejuu, Paje na Jambiani na kufanikiwa kumtia mikononi kijana huyo.
Alisema kijana huyo alikamatwa juzi majira ya saa 1:30 usiku wakati akiwa na misokoto hiyo katika mfuko wa kaki huko Bwejuu wakati akifanya biashara hiyo haramu.
Kamnda Hasaan alisema kijana huyo ni mzowefu wa uuzaji na msambazaji wa dawa hizo na kesi dhidi ya mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara tu taratibu za upelelezi zitakapokamilika.