NA HAJI NASSOR, PEMBA
MAHAKAMA ya Mkoa Chake Chake, imemtupa rumande hadi Agosti 20 mwaka huu, Mshitakiwa Bonifasi Maela Msalaba, kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka 16.
Mshitakiwa huyo, kabla ya kutupwa rumande, ilidaiwa mahakamani hapo naMwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Mohamed AliJuma alidai kuwa, alitenda kosa hilo mwezi Juni mwaka huu.
Mwendesha Mashtaka huyo mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Abull-razak Abdaull-kadir Ali, alidai kuwa, tukio hilo lilitokea siku na saaisiyofahamika, shehia ya Chambani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.
Alidai kuwa Mshitakiwa huyo, bila ya halali alimbaka mtoto wa miaka16, akijua kuwa yuko chini ya uangalizi wa wazazi wake, jambo ambaloni kosa kwani ni kinyume na kifungu cha 108 (1) (2) (e) nakifungu 109 (1) cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.
Mara baada ya kusomewa shtaka hilo, Hakimu wa mahakama hiyo Abdull-razak Abdull-kadiri Ali alimuuliza mshtakiwa iwapo ameyasikia maelezo ya shauri lake.
“Mshtakiwa umeyasikia maelezo ya kosa lako, sasa kwa vile kosa lako halina dhamana, utakwenda rumande hadi Agosti 20, mwaka huu na mashahidi waitwe,’’alisema. Hakimu huyo alimueleza mshitakiwa huyo, kwa vile upande wa mashtaka hawakuwasilisha mashahidi, ndio maana ameamua kuliahirisha shauri hilo hadi hiyo, mwaka huu.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mshitakiwa huyo Bonifasi Maela Msalaba miaka 20, alimbaka mtoto huyo mwenye miaka 16, jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 109 cha sheria hiyo, imebainisha kuwa, pindi mahakama ikimtia hatiani mbakaji, basi atatumikia kwa kipindi cha maisha Chuo cha Mafunzo au katika mazingira mengine atatumikia kifungo kisichopungua miaka 30.