NA ZAINAB ATUPAE

OFISI ya  Baraza la Sanaa,Sensa, Filamu na Utamaduni kwa kushirikiana na ofisi ya Hatimiliki Zanzibar (COSOZA), wamemsimamisha kwa muda mfanyabiashara wa duka la kuuza na kurikodi CD Omar Hassan, hadi pale atakapo maliza malipo  kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Fuoni Kibondeni baada ya kupita dukani hapo, wakati wa ziara ya kuwatembelea wasanii wakongwe hivi karibuni.

Dk. Omar Abdalla Adam alisema kwa mujibu wa sheria namba 7 ya mwaka 2015 imewalazimu kumsimamisha mfanya biashara huyo hadi pale atakapomaliza malipo yote.

Dk. Omar ambae pia ni Kaimu Kamishna Idara ya Utamaduni na Sanaa Zanzibar alisema, kinachotakiwa kwa wafanyabiasha wa CD kufanya kazi kwa utaratibu unaotakiwa kama serikali ilivyoelekeza.

Alisema ofisi yake haina tatizo na mfanya biashara yoyote ambaye atafuata utaratibu na sheria, ambapo ruhusa itatolewa  kuendelea na kazi yake ili kujipatia riziki na familia yake.