NA MARYAM SALUM, PEMBA

MAHAKAMA ya Wilaya Chake Chake chini ya hakimu wake, Ussi Khamis
Mjombo, imelazimika kuliahirisha shauri la kukashifu mwanamke
linalomkabili mtuhumiwa Awena Seif Mohamed (22), mkaazi wa Madungu,
kutokana na kukosekana kwa Hakimu husika   anaesikiliza shauri hilo.

Awali wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka
Zanzibar, Mohamed Ali Juma, alidai Mahakamani hapo kuwa shauri hilo
limefikishwa hapo kwa ajili ya usikilizwa, lakini  kwa vile Hakimu
husika wa shauri hayupo ni vyema likaahirishwa.

“Muheshimiwa shauri liliopo mbele yako linasikilizwa katika Mahakama
ya Mkoa chini ya hakimu Abdulrazak Abdulkadir Ali, lakini kutokana na
kutokuwepo kwa hakimu wa shauri hayupo, limeletwa mahakamani kwako kwa ajili ya kuliahirisha”, alidai.

Hakimu Mjombo, aliwaeleza watuhumiwa hao kwamba shauri lao linasikilizwa
katika mahakama ya mkoa chini ya hakimu huyo
ambapo limeletwa  kwa ajili ya kuahirishwa na ni vyema wahusika  kuwa
wastahamilivu kutokana dharura ya hakimu hadi Septemba 14 mwaka huu.

Mwendesha Mashitaka huyo alidai kuwa mtuhumiwa anakabiliwa na tuhuma
za kumkashifu mwanamke mwenzake, na kudai kuwa ametoa video za uchi ambapo kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 114(3) sheria ya adhabu  namba 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.

Ilidaiwa kuwa shauri  hilo limetendeka Machi 22 mwaka huu mjira ya
saa 2:00 asubuhi  shehia  ya Madungu Wilaya ya Chake  Chake, ambapo Hakimu  huyo alitahadharisha siku hiyo mashahidi  wanaohitajika kufika wafike.