BARCELONA, Hispania

PHILIPPE COUTINHO anakaribia kuhamia rasmi Ligi Kuu soka ya  England  na kujiunga na miamba wa London Kaskazini Arsenal, kwa mujibu wa wakala wake ambaye pia anadai kuwa uhamisho wa kiungo huyo wa kati wa Barcelona unakaribia kukamilika.

Coutinho ameshindwa kuonyesha thamani ya pauni milioni 145 iliyotumiwa kununuliwa akihamia Camp Nou akitokea Liverpool wakati wa dirisha la uhamisho la Januari mwaka 2018.

Winga huyo wa Brazil alitumia msimu mzima akiwa na mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich kwenye mkataba wa mkopo lakini alishindwa kupata mkataba wa kudumu ugani Allianz Arena.

 Mchezaji huyo sasa anahusishwa na klabu kadhaa vya Ligi Kuu kufuatia rekodi aliyoandikisha na Liverpool zamani.