ZASPOTI
KLABU ya Arsenal inapanga kusajili wachezaji wawili zaidi baada ya kumnasa kiungo wa Chelsea, Willian kwa uhamisho wa bure.
Washika bunduki hao watasimamia juhudi za kumleta, Thomas Partey kutoka Atletico Madrid, na pia wako kwenye soko la beki mwengine.

Lakini wakati Mkurugenzi wa Ufundi, Edu, anadai kwamba Willian ni mwanzo tu wa mchakato mkubwa, alionya pia kuwa kutakuwa na mauzo katika msimu huu wa joto.

Arsenal inamtaka kiungo huyo Ghana kujiunga nao, lakini, hawatolipa kipengele chake cha kutolewa kwa pauni milioni 45.

Washika bunduki wataongeza kasi ya kumleta mchezaji wa miaka 27 sasa Atletico Madrid wako nje ya Ligi ya Mabingwa lakini wanahitaji bei ya kuuliza ishuke.
Arsenal imemsajili Willian kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya mkataba wake na Chelsea kukamilika.

Chelsea ilitoa ofa yake mpya kwa mchezaji huyo, lakini, haikuifikia iliyotolewa na Arsenal.
Willian alicheza michezo 339 akiwa Chelsea baada ya kusajiliwa akitokea klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi kwa pauni milioni 30 mwaka 2013.

Arsenal ilimaliza nafasi ya nane katika Ligi Kuu ya England msimu uliopita, huku Chelsea ikimaliza ya nne na kupata nafasi ya kushiriki katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hata hivyo, Arsenal iliwashinda mahasimu wao wa Uingereza katika fainali ya Kombe la FA mechi ambayo Willian hakucheza kwa sababu ya maumivu, ili kuhakikisha inajipatia nafasi katika mechi za Ligi ya Ulaya.

Willian anafuata nyayo za mlinzi David Luiz aliyehama Chelsea na kujiunga na Arsenal Agosti mwaka jana.
Mkurugenzi wa kiufundi katika klabu ya Arsenal Edu alisema: “Namfahamu vizuri, kwa kipindi kirefu kwa sababu tumekuwa tukifanyakazi pamoja katika timu ya taifa ya Brazil.(AFP).