MADRID, Hispania

DIEGO Carlos beki wa Sevilla anatajwa kuingia anga za Arsenal kujiunga ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu wa 2020/21.

Arsenal iliyo chini ya kocha Mkuu, Mikel Arteta anatajwa kukumkosha Arteta ambaye ametwaa taji la FA kwa kuitungua mabao 2-1 Chelsea Uwanja wa Wembley.

Kwa mujibu wa ripoti Arsenal ni namba moja kuonyesha nia ya kumpata beki huyo raia wa Brazil.

Dau la beki huyo linatajwa kuwa pauni milioni 68 ili aachiwe ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki La Liga ili aibukie ndani ya Ligi Kuu England.