MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Venance Mabeyo, ameongoza Gwaride maalumu la heshima la kuwaaga Maafisa 16 wa ngazi za juu wa Jeshi waliostaafu.

Gwaride hilo limefanyika jijini Dar es Salaam ambapo Luten Jenerali mmoja Meja Jenerali Sita na mabrigedia Jenerali tisa.

Nae Mmoja wa wastaafu, Luten Jenerali (Mstaafu), Paul Massao, amesema kutumikia jeshi ni kazi ambayo ni yakujitolea inamuhitaji mtu aliekuwa mzalendo wa nchi yake na asiejali maslahi binafsi.

Aidha Massao, amesema kuwa jeshi ni mali ya Wananchi hivyo wanatakiwa kutoa ushirikiano wakutosha, ili kuweza kukabiliana na vita baridi ya vikundi vya watu wasiotakia mema Tanzania.

Kwa upande wake Brigedia Jenerali (Mstaafu), Mary Hiki amesema jeshi linamisingi na taratibu zake, ukizifuata utaishi muda mrefu jeshini na kustaafu kwa heshima.