LONDON, England

KOCHA wa Aston Villa, Dean Smith anakusudia kukiimarisha kikosi chake katika safu ya ushambuliaji baada ya kufanikiwa kuepuka kushuka daraja.

 Katika kuhakikisha inafanikiwa katika hilo, wamekusudia kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, raia wa Ubelgiji Divock Origi, 25.

Origi amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 44 pekee ndani ya Liverpool msimu huu uliyomalizika, lakini mara zote amekuwa mtu wa kusugua benchi akiwapisha Mo Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino wakianza.