LONDON, England
NAHODHA wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang, amekubali kusaini dili jipya la miaka mitatu Emirates.

Nyota huyo alikuwa kwenye mpango wa kuondoka kwa washika bunduki hao wanaonolewa na kocha mkuu, Mikel Arteta, lakini, sasa ameonyesha nia ya kuendelea kukitumikia kikosi hicho kwa ajili ya msimu wa 2020/21.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa raia wa Gabon sasa anatarajiwa kulipwa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki.

Pia, Arsenal inapiga hesabu za kupata saini ya beki wa Lille, Gabriel Maghalhaes ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho.

Arteta anahitaji kufanya mabadiliko makubwa katika kujenga timu bora kwenye Ligi Kuu ya England pamoja na michuano mengine ya Ulaya.(Goal).