NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KLABU ya soka ya Azam FC inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara, jana imefanya tamasha kubwa la Azam Festival.

Tamasha hilo lilianza mapema asubuhi na kuambatana na utambulisho wa jezi zao, ambazo zitatumika kwenye msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara.

Katika jezi zilizotambulishwa jezi nyeupe itatumika nyumbani huku bluu na rangi ya chungwa zikitumika ugenini.

Kilele cha tamasha hilo itakuwa Agosti 23 wiki ijayo huku mgeni rasmi akiwa ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Akizungumza na Zanzibar Leo uwanjani hapo Ofisa Habari wa klabu hiyo Abubakar Zakaria ‘Zakazakazi’, alisema kwa mara timu yao inafanya hivyo na wamefurahi kulifanikisha hilo.

Alisema wananchi wamelipokea jambo hilo na kulifanya la kwao hivyo ni hatua nzuri na jambo ambalo watakuwa wanalifanya mara moja kwa kila mwaka.

‘ Kilele chetu kitakuwa Jumapili ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,” alisema.