NA KHAMISUU ABDALLAH

BARAZA Kuu la Umoja wa Vijana CCM Taifa (UVCCM) jana limefanya uchaguzi wa kuwateuwa viongozi katika ngazi ya vijana ambao watawakilisha vijana katika Baraza la Wawakilishi na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akitangaza matokeo hayo kwa nafasi ya Uwakilishi katika uchaguzi uliofanyika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dodoma, Msimamizi wa Uchaguzi Kombo Hassan Juma, alimtaja Salha Mohammed Mwinjuma kutoka Mkoa wa Kusini Unguja aliepata kura 66 na nafasi ya pili ilishikiliwa na Khudhaima Mbaraka kutoka wilaya ya Mjini aliepata kura 50.

Kombo ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa alisema katika nafasi hizo mbili wagombea wote walikuwa saba.

Kwa nafasi nne za ubunge wajumbe waliotoka Zanzibar mkutano huo ulimchagua Munira Mustapha Khatib kutoka Kusini Pemba kwa kura 88 akifuatiwa na Latifa Khamis Juakali kutoka Kusini Unguja kura 84, Amina Bakar Yussuf Kaskazini kura 79 na nafasi ya nne ilishikiliwa na Amina Ali Mzee aliepata kura 73 kutoka wilaya ya Mjini ambapo wagombea wote walikuwa sita.

Kwa Tanzania bara wagombea wote walikuwa 29 na waliochaguliwa kwa nafasi sita walikuwa ni Lulu Mwacha kwa kura 77 anaetokea Arusha, mshindi wa pili ni Halima Abdalla Bulembo aliepata kura 74 anaetokea Mara akifatiwa na Juliana Didas Masaburi aliepata kura 70 anaetokea Simiyu.

Nafasi ya nne ilishikiliwa na Lucy John Sabu aliepata kura 48 na nafasi ya tano na sita zilishikiliwa na Asia Abdulkarim Alamba kutoka Manyara na Judith Kapanga Saidu kutoka Ruvuma waliopata kura 33 kila mmoja.  

Msimamizi huyo alisema majina hayo yatapelekwa katika ngazi za juu za chama ikiwemo Kamati kuu na Halmashauri kuu ya CCM Taifa hivyo wagombea hao wakumbuke kuwa bado mchakato unaendelea.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Tanzania, Kheir Denis James, aliwaomba wajumbe hao kushirikiana pamoja katika kuendeleza umoja wao baada ya uchaguzi huo kwani ndio nguzo imara itayowawezesha kuimarika kwa jumuiya yao

Hata hivyo, aliwasisitiza wananchi wote ambao wamejiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi na kukipigia kura Chama cha Mapinduzi ili kiendelee kushika dola katika nafasi zote ikiwemo ya Urais, Ubunge, Uwakilishi na Madiwani.  

Katika mkutano huo wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana CCM Taifa (UVCCM) ulikuwa na wajumbe 109 kura zilizoharibika