MINSK,BELARUS
BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya mazungumzo kuhusu mgogoro unaondelea nchini Belarus na kutoa wito wa kuzuia mzozo huo kuenea.
Estonia na Marekani ndizo zilizoomba majadiliano hayo wakati China ikisema kinachoendelea Belarus sio suala la Baraza la Usalama.
Nao viongozi wa Umoja wa Ulaya walimuhimiza Rais Vladmir Putin wa Urusi kushinikiza mazungumzo katika taifa jirani la Belarus, wakati wafuasi wa upinzani wakiendelea kupinga ushindi wa Rais Alexander Lukashenko .
Maelfu ya waandamanaji walikusanyika katika uwanja wa uhuru wakimshinikiza Lukashenko kujiuzulu.
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani alimueleza Putin kwamba viongozi wa Minsk lazima waingie katika majadiliano ya kitaifa na wapinzani na jamii ili kuondokana na mgogoro huo.