NA MWAJUMA JUMA

TIMU ya mpira wa Kikapu ya Beit El Ras imeshuka daraja katika msimu wa 2020/2021, wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja.

Beit El ras ilimaliza ikiwa na pointi saba sawa na timu za New West na Usolo, baada ya kulingana kwa pointi ilizidiwa kwa  idadi kubwa ya mabao ya kufungwa.

Hivyo wakati timu hiyo imeshuka timu mbili zilizobakia za  New West na Usolo ,zimenusurika kushuka daraja  na msimu ujao kuendelea kucheza ligi hiyo. Bei El ras baada ya kushuka, sasa itasubiri kucheza ligi B ambayo inatarajiwa kuanza Agosti 15, mwaka huu na itakuwa ikichezwa uwanja wa Mao  Zedong .