MINSK,BELARUS

KIONGOZI  wa upinzani nchini Belarus Svetlana Tikhanovskaya amewataka waandamanaji wanaodai demokrasia kuendelea na juhudi hizo, akisema Rais Alexander Lukashenko hana chaguo ila kuzungumza na upinzani.

Katika mahojiano na shirika la habari la AFP, Tikhanovskaya pia alisema watu wa Belarus wameondoa hofu yao na kuiita hatua ya Lukashenko ya kuongeza usalama katika mipaka kuwa ni juhudi tu za kutaka kuondoa mtazamo katika matatizo ya ndani ya nchi hiyo.

 Wapinzani wa Alexander Lukashenko kiongozi aliyekuwapo madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Ulaya wanaendelea kuandamana katika taifa hilo la zamani la Umoja wa Kisovieti kupinga kuchaguliwa kwake tena na wanadai ajiuzulu.