BETTY Bigombe alizaliwa Oktoba 21 mwaka 1952, alikulia kaskazini mwa Uganda na mwisho, ambapo kwa siku moja alilazimika kutembea umbali wa maili nne akifuata masomo skuli.
Betty Bigombe alikuwa mtoto wa nane kuzaliwa kati ya watoto 11, ambapo alikuwa katika wilaya ya Gulu katika jamii ambayo utamaduni ambao inapenda sana kutunza utamaduni wake hadi hivi sasa.
Akiwa binti mdogo akibisa chini ya uangalizi wa wazee wake, alieelewa vyema na kuufanyia kazi ule msemo usemao elimu ni ufunguo wa maisha. Hivyo alijitahidi sasa kutafuta elimu pamoja na kukabiliwa na chungu ya changamoto kama mabinti wengine wanaotokea kwenye familia masikini.
Kwa hakika jitihada zake zimesaidia kwani alikuwa mmoja wa wanafunzi hodari darasani kiasi cha kufanikiwa kujiunga na chuo kikuu cha Makerere kufanya shahada yake ya kwanza sayansi ya jamii na kufanikiwa kufanya shahada ya pili ya utawala wa umma.
Alieleza kuwa hakuwa rahisi kwa familia yake kumsomesha bali ilipata msaada wa kifedha kutoka kwa kanisa wakati alipokuwa akiendelea na masomo yake.
“Bila elimu, pengine huenda nisingelikuwa hapa na huenda ningelikuwa na watoto 20 na kuishi vijijini nikifanya kazi ya malezi na nyengine ngumu, kama vile kuzalisha chakula cha familia kwa kulima”, alisema.
Furusa hiyo aliyoipata kutoka katika kanisa ya kupewa fedha za masomo ilimuwezesha kupata ufadhili wa masomo ya elimu ya juu zaidi katika chuo kikuu cha Harvard mnamo mapema miaka ya 1980, alirejea nyumbani akiwa ameolewa na watoto wawili.
Miaka 30 baadae jukumu la Betty lilikuwa la kuamua hatma ya siku zijazo za eneo zima ya wilaya ya Gulu, ambapo alichukua jitihada za kufanya jaribio kushauriana na mbabe hatari wa kivita Joseph Kony, kiongozi wa waasi wa Lord’s Resistance Army.
Wakati anarejea Uganda aliikuta nchi yake ikiwa imetumbukia kwenye vita ambapo vikosi vya rais Milton Obote vilikuwa vikikabiliana na vuguvugu lililokuwa likiongozwa na Yoweri Museveni.
“Wakati huo, nilikuwa nikiwaficha baadhi ya watu waliokuwa wakimuunga mkono rais Museveni. Nilifanya kazi na mwanamke mmoja raia wa Ujerumani aliyekuwa akihudumu katika shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR na tulisaidia kuwasafirisha watu waliokuwa hatariri nchini Kenya. Ukiwa na bendera ya UN, ni rahisi. tuliweza kupita vizuizi vya barabarani na kuwafikisha mahali salama, hali iliyowafanya watu kupigania haki zao.”
Mnamo mwaka mwaka 1986, Museveni alifanikiwa kuwa rais, wadhifa anaoshikilia hadi wa leo. Alimzawadia Betty kwa kumfanya waziri wa serikali.
“Nilipata usumbufu sana nilipoteuliwa katika wadhifa wa uwaziri kwa sababu mawaziri wengi walikuwa wanaume. Kile walichoniagiza kufanya ni kusoma makaratasi”, alisema.
Kutokana na hali hiyo alieleza kuwa alimfahamisha rais kuwa anataka kujiuzulu kwa sababu hakuona chochote cha msingi ch akufanya isipokuwa kusoma vitabu wakati alitaka kufanya kazi.
Betty alisema kutokana na hali hiyo, rais alishangaa sana kusikia kuwa nataka kujiuzulu na kumueleza kuwa mawaziri wa Afrika hawajiuzulu, hususan wanawake.
Kwa hivyo Betty alikuja na pendekezo la kukutana na waasi kaskazini mwa nchi Lord’s Resistance Army, baada ya mapigano kuzuka ili kufahamu walichokuwa wakipigania na mahali walipoweka silaha zao.
Museveni alikubaliana na pendekezo hilo, lakini akamuomba Bigombe kuwashawishi waasi kukomesha mapigano. Ndugu jamaa na marafiki zake walihofia mpango huo kwani ulikuwa hatari kwa maisha yake.
“Watu wengi waliniambia niachane na mpango huo, ‘anataka ufariki.’ Marafiki waliniambia, ‘Hiyo si kazi ya wanawake. Kwanini amekupatia jukumu hilo? Hujawahi kuifanya.'”
Bila shaka ni wazi kuwa hakuna mtu aliyekuwa mjasiri wa kutosha kuzungumza na Joseph Kony, kiongozi wa kundi hatari la Lord’s Resistance Army (LRA).
Jaribio lake la kwanza kukutana na waasi wa Lord’s Resistance Army lilikuwa la kutisha kwani LRA walimpa barua Betty wakieleza kuwa Museveni amewatukana kwa kumtuma mwanamke kujadiliana nao.
Awali walitishia kumuua lakini hakutishika na alijitolea kuhakikisha mapigano yanakomeshwa. Baadae walimtuma mtu aliyetekwa na kundi la Kony kuwasilisha barua ya pili ana kwa ana.
Mtu huyo alijitokeza na sijui aliponea vipi kifo. Hakua na chanjo ya surua, amekatwa sehemu ya mdomo na viungo vyake na alikuwa ameroa damu ambapo abarua aliyokuwa nayo imetumwa kwangu Betty na imejaa damu.
Bila uwoga, Betty aliamua kumwandikia barua Kony, alimtaja kama mwanangu na kutumia njia za kidini kuwasiliana nae na kuomba wakutane. Hatimae Kony alikubali kukutana nae, alihofia huenda akaamua kumtesa na kumuua badala kukubali atumiwe kama chambo cha kumkamata.
Kwa mara ya kwanza alikutana na Kony ndani ya kichaka kikubwa chenye kutisha. “Alikuwa chini ya ulinzi mkali, muziki wa kidini ulikuwa ukicheza, kulikuwa na wanaume waliovalia nguo za watawa na walikuwa wamejihami kwa bunduki”, alisema Betty.
Walikuwa wakiimba muziki wa kidini, unaosema kwamba ushetani unakaribia kuwatoka. Mandhari hayo yalikuwa ya kushangaza. Alikuwa amevalia sare za kijeshi na alikuwa tayari kuniogofya.
Miezi 18 baada ya wao kukutana ana kwa ana mara kadhaa Kony, alianza kumuita Betty “Mummy Bigombe”. Na hatimae alikubali kutoka mwituni kufanya mazungumzo ya amani na rais Museveni.
Betty alikwenda kukutana na rais ili wakubaliane mashariti yatakayooongoza mazungumzo hayo ya amani.
Badala kufikia wakati huo mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai, ICC ilikuwa imemfungulia Kony mashtaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.
Kazi ya Betty ilikua msingi wa mazungumzo ya amani nchini Sudan Kusini mwaka 2006, japo yalivunjika dakika za mwisho, baada ya Kony kukataa kutia saini mkataba wa amani.
Hivyo Museveni alimtishia Kony hadharani na kutangaza katika mkutano wa hadhara kuwaajitokeze mara moja la sivyo akabiliwe vikali na vikosi vya serikali.
Kony na vikosi vyake walijibu kwa kutekeleza mashambulizi mabaya katika kituo kimoja karibu na mpaka wa Uganda na na Sudan ambapo watu 300 waliuawa kinyama.
Hapo ndipo Betty alipojiuzulu kama mpatanishi mkuu na hivyo kuelekea Marekani. “Nilisikitika sana nikalia kwa machungu ndani ya ndege. Sikuamini Tulivyoshindwa kufikia amani, lakini yote haikuwa nawahurumia watu waliokuwa wakiteseka bila sababu,” alisema.

Alirejea tena kwa masomo Chuo Kikuu cha Harvard na baadae kuajiriwa na Benki ya Dunia mjini Washington. Asubuhi moja mwaka 2004 alifungua televisheni kutazama yanayojiri lakini ghafla alipana na taarifa iliyobadilisha kila kitu.
Kulikuwa na tarifa katika kituo cha habari cha CNN – Kwamba waasi wa Lord’s Resistance Army walivamia kambi moja ya wakimbizi na kuua zaidi ya watu 300.
“Baada ya hapo niliona picha yangu – ikiandamana na maandishi – Mtu pekee aliyekaribia kukomesha mapigano, mtu pekee aliyekutana na kiongozi wa waasi. Ujumbe huo nilihisi ni wito kwangu”, alisema.
Betty alirejea Uganda na kujaribu kupanga tena mkutano baina yake na kiongozi wa waasi wa LRA, Joseph Kony, hata hivyo alihofia hatua ya serikali ya Uganda kufadhili mpango huo utaathiri msimamo wake kwa hivyo aliamua kutumia pesa zake binafsi.
Hivi sasa Betty ni Mkurugenzi wa kitengo cha kushughulikia mizozo katika Benki ya Dunia, amezuru maeneo tofauti duniani kutoa mafunzo kwa wapatanishi na kuwafahamisha alichojifunza alipokutana na waasi wa LRA mwituni.