WAPIGA kura nchini Marekani wataamua Novemba 3 iwapo rais Donald Trump ataendelea kubakia ikulu ya Whitehouse kuongoza muhula mwingine wa miaka minne ama atafungasha virago kumpisha rais mpya.
Rais huyo kutoka cha Republican anapingwa na mgombea wa chama cha Democratic, Joe Biden, ambaye alikuwa makamu wa rais wakati wa utawala wa rais Barrack Obama, lakini amekuwa katika siasa za Marekani tangu mwaka 1970.
Huku siku ya uchaguzi ikikaribia, kampuni za kura ya maoni zitajaribu kupima hisia za wananchi wa taifa hilo kwa kuwauliza ni mgombea yupi wanayempenda na wangependa awaongeze katika kipindi chengine cha miaka minne ijayo.
Kura za maoni ni muongozo mzuri kuhusu umaarufu wa mgombea nchini, lakini sio moja kwa moja zinaweza kutabiri matokeo ya uchaguzi.
Kwa mfano mnamo mwaka 2016, Hillary Clinton aliongoza katika kura za maoni na kuibuka mshindi kwa kura milioni tatu zaidi ya mpinzani wake Donald Trump, lakini uchaguzi ulipofanyika akashindwa kwasababu raia wengi wa Marekani hupiga kura kwa kutumia njia ya posta hivyo basi ushindi wa kura nyingi hauwezi kukusaidia kushinda uchaguzi.
Katika uchaguzi wa mwaka huu Joe Biden kwa muda mrefu anaongoza kwenye kura za maoni dhidi ya Trump, lakini hicho pia kinaweza kisiwe kigezo cha ushindi.
Biden amekuwa akijipatia asilimia 50 katika wiki za hivi karibuni na amekuwa akiongozi kwa pointi 10 mara kadhaa lakini Trump amejitahidi na kuweza kuongeza umaarufu wake katika siku chache zilizopita.
Tofauti ni kwamba mwaka 2016, kura hizo hazikuwa wazi kama ilivyo sasa na ni asilimia ndogo iliyowatawanya Trump na mpinzani wake wa Democrat, Hillary Clinton kwa alama kadhaa wakati uchaguzi ulipokuwa ukikaribia.
Ni Majimbo gani yatakayoamua mshindi?
Katika uchaguzi uliopita Clinton aligundua kwamba idadi ya kura unazoshinda sio muhimu zaidi ya eneo unalopata kura hizo.
Majimbo mengi hupiga kura wakimchangua mgombea kutoka chama kilekile, ikimaanisha kwamba kuna majimbo machache ambayo wagombea wana fursa ya kushinda.
Haya ndio maeneo ambayo uchaguzi utashindiwa na kupotezwa kama majimbo yanayogombaniwa. Katika mfumo wa uchaguzi wa Electoral College, unaotumiwa na Marekani kuchagua rais wake, kila jimbo hupatiwa idadi ya kura kutokana na idadi ya watu. Takriban kura 538 za Electoral College zilizopo zinawaniwa hivyo basi kila mgombea anahitaji kushinda kura 270.
Nani anayeongoza katika majimbo yanayowaniwa?
Hadi sasa, kura za maoni katika maeneo yanayowaniwa zinamuonesha Joe Biden akiwa kifua mbele, lakini kuna muda mwingi kabla ya uchaguzi huo kufanyika na huenda mambo yakabadilika haraka, hususan wakati Donald Trump atakaposhirikishwa.
Kura hizo za maoni zinasema kwamba Biden anaongoza katika jimbo la Michigan, Pennsylvania na Wisconsin – majimbo matatu ambayo mpinzani wake wa Republican alishinda kwa tofauti chini ya asilimia moja ili kupata ushindi 2016.
Tofauti ya ushindi wake katika jimbo la Iowa, Ohio na Texas ilikuwa kati ya asilimia 8 -10 wakati huo, lakini kwa sasa yuko sawa na Biden katika majimbo yote matatu kufikia sasa.
Kura hizo za maoni zinaweza kusaidia kuelezea uamuzi wake kumbadilisha meneja wake wa kampeni mwezi Julai na tamko lake la mara kwa mara la ‘kura za maoni bandia’.
Masoko ya kamari, hata hivyo hayajamfutilia mbali rais Trump katika fursa tatu za hivi karibuni masoko hayo yanampatia rais Trump ushindi wa fursa moja mnamo mwezi Novemba.
Mkosi wa rais Trump unawafanya wapinzani wake kuwa thabiti.
Mlipuko wa virusi vya corona umetawala vichwa vya habari nchini Marekani tangu kuanza kwa mwaka huu na hatua zilizochukuliwa na rais huyo zimegawanya hisia kulingana na vyama.
Wanaounga mkono siasa yake waliongezeka katikati ya mwezi Machi baada ya kutangaza hali ya tahadhari na kutoa dola bilioni 50 katika majimbo kuzuia kusambaa kwa maradhi hayo.
Wakati huo, asilimia 55 ya Wamarekani waliunga mkono hatua yake, kulingana na data za Ipsos, kampuni kubwa ya kura ya maoni duniani.
Lakini uungwaji mkono wowote alioupata kutoka kwa Democrats ulipotea baada ya hatua hiyo huku wafuasi wa Republican wakiendelea kumuunga mkono rais wao.
Hata hivyo, data ya hivi karibuni inaonesha kwamba hata wafuasi wake wameanza kuhoji hatua yake ya kukabiliana na maradhi hayo huku majimbo yaliyo Kusini na Magharibi ya taifa hilo yakikumbwa na mlipuko mpya wa virusi hivyo.
Uungwaji mkono wa Republican umepungua hadi asilimia 78 kufikia mapema mwezi Julai.
Hii ndio sababu katika siku za hivi karibuni amekuwa akijaribu kubadilisha ujumbe wake kuhusu virusi vya corona, akibadilisha tamko lake kwamba virusi hivyo vitatoweka na kuonya badala yake kwamba hali itakuwa mbaya kabla ya kuimarika.