NA ZAINAB ATUPAE
WASANII nchini wameshauriwa kuvaa mavazi ya stara wakati wanapofanya kazi zao.
Ushauri huo umetolewa na msanii mkongwe wa maigizo Mwema Khamis Juma (Binjiwa), huko Mwera wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema wasanii wa sasa hufanya mambo ambayo ni kinyume na maadili yao.
Alisema wasanii wa zamani walikuwa wakifanya kazi zao kwa kufuata maadili yao kama inavyotakiwa, na hiyo ndio sababu iliyowafanya wananchi wengi kuwa na hamu ya kuangalia kazi zao.
Alisema ni vyema wazazi ambao vijana wao wanajishughulisha na kazi za Sanaa kukaa nao na kuwafahamisha maadili yanavyotakiwa ili waache kuiga utamaduni wa nchi nyingine.
Aliwataka viongozi wa Baraza la Sanaa,Sensa,Filamu na Utamaduni Zanzibar kuangalia maadili wakati wasanii wanapotoa kazi zao.