NA SHITA HUSSEIN MIHAMBO

MADEREVA  wanaotoa huduma za Boda boda katika Wilaya ya Katiwametakiwa kutii sheria za nchi na maagizo yanayotolewa na viongozi wa Serikali hususani katika suala zima la uendeshaji vyombo kwa manufaa yao na wananchi  .

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kati , Hamida Mussa Khamis,wakati wa kikao maalum cha waendesha  boda boda wa Wilaya hiyo hapo katika ukumbi wa TC Dunga.

Amesema kumekuwa na wimbi kubwa la ajali ambazo husababishwa nawaendesha  boda boda, jambo  ambalo linasababisha kukatisha maisha watu na  wengine kupoteza viungo na kusababisha  ulemavu wa kudumu

Hamida amefahamisha kuwa kikao hicho kitasaidia kuwajua waendesha boda boda wote wa Wilaya hiyo, kwa kuwafanyia  vitambulisho na vikoti maalum, vitavyoonesha majina yao na kituo wanachofanyia kazi hivyo itasaidia kujua wageni wanaoingia katika  maeneo mengine kwa kufanya mambo yasiofaa. 

Washiriki kutoka Jeshi la Polisi Mkuu wa Usalama barabarani Mkoa wa Kusini Inspekta Rashida Rashid Abdalla na Inspekta Ramla Aley wamewataka watoa huduma za boda boda kufuata sheria na taaratibu haswa kipindi hiki cha kuelekea katika kampeni za Uchaguzi mkuu na kusema kuwa hawatosita kuwachukulia hatua wale wote watakaokiuka sheria za Usalama barabarani.