NA ZAINAB ATUPAE

TIMU ya Bwejuu Mjini na Tupogo juzi zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bao 1-1, ikiwa ni ufunguzi wa mashindano ya Bwejuu Super Cup.

Mtanange huu uliopigwa uwanja wa BZL majira ya saa 10:00 jioni, ambao uliokuwa wa ushindani kwa timu hizo,huku mashabiki wakijaa uwanjani hapo.

Mchezo huo uliokuwa wa ushindani kila mmoja kusaka pointi tatu ambazo zitamuweka katika sehemu nzuri kwenye msimamo wa mashindano hayo, dakika ya 17 Tupogo iliweka  bao lililofungwa na Hassan Ameir.

Bao la kusawazishwa la Bwejuu  Mjini lilifungwa  Amour Haji Hassan dakika ya 39, ambayo yalidumu hadi mwisho wa mchezo huo.

Katika mashindano hayo mgeni rasmi alikuwa Sheha wa Shehiya ya Bwejuu Maryam Pandu Kweleza na  alizitaka timu zilizoshiriki mashindano hayo, kuwa kitu kimoja na kucheza kwa nidhamu, kwani nidhamu ndio jambo la msingi ambalo litasadia kufikia malengo yao.