LONDON, England

DANI CEBALLOS ameiambia Real Madrid kwamba hataki kurudi katika klabu hiyo inayonolewa na kocha Zinedine Zidane kufuatia ushindi wa Arsenal dhidi ya Chelsea kwenye fainali ya Kombe la FA.

Kiungo huyo amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Mikel Arteta wakati wa mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza na alitoa mchango mkubwa kuwasaidia kushinda kombe la FA kwa mara ya 14 kwenye historia ya klabu.

Arteta ana hamu ya kumbakisha Ceballos kwenye klabu na sasa lazima Arsenal ijadili mpango mpya wa mkopo na Real Madrid.

Akiongea baada ya ushindi wa Kombe la FA la Arsenal, Ceballos alifafanua kwamba atafanya mazungumzo na Rais wa Madrid, Florentino Perez kujadili hatma yake baada ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Klabu Bingwa ya Uhispania mwezi huu.

‘Hivi sasa nimefurahi, lakini ni wakati wa kupumzika nyumbani na familia yangu, na rafiki yangu wa kike, ambaye sijawaona kwa muda mrefu, nimekuwa peke yangu London kwa miezi mitano au sita, kwa hivyo sasa ni wakati kuwa pamoja nao na kutafakari juu ya siku zijazo.

‘Ikilinganishwa na klabu yoyote duniani, Real Madrid ndio bora zaidi, lazima tusubiri tuone kama watarudi dhidi ya Manchester City na tutashughulikia mustakabali wangu baada ya hapo’’.

Ceballos pia alikulia Real Betis, ambaye alijiunga nayo mwaka 2011 kabla ya kununuliwa na Real Madrid mnamo 2017, pia wameendelea kuwasiliana naye msimu huu kwani pia wako tayari kumsaini kwa mkopo msimu huu wa joto.

‘Ninaipenda sana Betis, kwa wale wote ambao wanafanya kazi kwa ajili ya klabu, ambao wanajua mapenzi niliyonayo kwao na wamewasiliana nami msimu wote,’ alisema kiungo huyo.